Kibadilishi sarafu

Je, unahitaji ugeuzaji sarafu wa haraka? Weka tu maelezo kwenye kibadilishi sarafu chetu rahisi. Utapata viwango vya hivi punde kila wakati kwani kibadilishi fedha chetu husasishwa katika muda halisi.

Jinsi Kibadilishi Sarafu kinavyofanya kazi

Ili kuanzisha ugeuzaji mpya, fuata hatua hizi:

  • Chagua sarafu yako ya msingi kutoka kwenye orodha yoyote kati ya orodha 6 kunjuzi

  • Chagua hadi sarafu zingine 5

  • Weka kiasi cha sarafu ya msingi

  • Na viwango vya ubadilishaji vitakokotolewa kiotomatiki

Ikiwa ungependa kubadilisha sarafu yoyote, chagua tu sarafu unayotaka kutoka kwenye orodha kunjuzi.

Maswali yanayoulizwa sana

Viwango vya ubadilishaji hubainishwa na kiwango cha kuelea au kiwango kisichobadilika.

Viwango vya kuelea hukokotolewa kulingana na usambazaji na mahitaji kwenye masoko ya kimataifa. Mahitaji makubwa ya sarafu yataongeza thamani yake huku mahitaji ya chini yatashusha bei.

Kwa upande mwingine, kiwango kisichobadilika ni wakati sarafu inapowekwa dhidi ya sarafu nyingine kuu, kama vile yen ya Japani au dola ya Marekani, na serikali kupitia benki yake kuu.

Hakuna siku mahususi ambayo ni wakati mzuri wa kubadilishana sarafu kwani bei ya forex hutegemea mambo mengi, kama vile matukio ya kiuchumi na kisiasa, taarifa za habari, imani ya wawekezaji na mengine mengi.

Kibadilishi sarafu ambacho kinasasishwa kwa wakati halisi, kama vile Kibadilishi Sarafu cha Exness, kinafaa zaidi kwa kujua viwango vya ubadilishaji vilivyosasishwa.

Boresha jinsi unafanya biashara

Jionee mwenyewe kwa nini Exness ndiye broker anayefaa zaidi kwa traders zaidi ya 800,000 na washirika 64,000.