Kalenda ya Kiuchumi

Fuatilia habari zenye athari kubwa, matukio muhimu ya kiuchumi yanayoathiri soko na matoleo ya data ukitumia Kalenda yetu ya Kiuchumi. Alamisha ukurasa huu na urejelee kalenda mara kwa mara ili kusasisha matukio katika masoko ya fedha.

Saa

Ishara

Tukio

Halisi

Ubashiri

Iliyotangulia

Panga biashara yako ukitumia kalenda ya kiuchumi ya Exness

Kuhusu Kalenda ya Kiuchumi

Kalenda ya Kiuchumi ni kipengele kinachosaidia traders kufuatilia na kuchanganua matukio ya soko, na kubashiri mienendo zaidi ya bei. Inaangazia habari zijazo za kitaifa na kimataifa kote ulimwenguni kwa mpangilio kulingana na tarehe.

Matukio haya makuu yanaweza kuwa na athari kubwa kwenye masoko ya fedha na kwa kawaida hutangazwa au kutolewa katika ripoti. Mifano ya matukio kama haya ni pamoja na maamuzi ya sera za fedha, indicators za kiuchumi, matangazo ya Pato la Taifa (GDP), nambari za Malipo ya Mashirika Yasiyo ya Kilimo (NFP), maamuzi ya viwango vya riba na mengine mengi.

Huwa tunawaarifu wafanyabiashara kabla ya matukio, habari na matoleo ya data yajayo ili kuwafahamisha kuhusu saa na instruments ambazo zinaweza kuathiriwa. Unaweza kupata arifa hizi chini ya kichupo cha "Mailbox" kwenye jukwaa lako la biashara. Tafadhali kumbuka kuwa athari za habari za kiuchumi na indicators zinaweza kutofautiana kwa kila instrument.


Kwa nini unapaswa kutumia Kalenda ya Kiuchumi

Kalenda ya Kiuchumi ni muhimu sana ikiwa ungependa kufuatilia habari, ripoti na matangazo yajayo kwa muhtasari.

Matukio haya yanaweza kuathiri sana kubadilikabadilika ghafla kwa jozi za sarafu ya forex, stocks na masoko mengine. Kwa hivyo, traders mara nyingi hutumia kalenda kupanga trade zao na kujulishwa kuhusu mifumo ya chati na indicators ambazo zinaweza kuathiriwa na matukio.

Kwa kuwa matukio yanaweza kusababisha ongezeko la bei wakati wa uchapishaji, ni mazoea mazuri kurejelea kalenda kabla ya siku ya kutrade.


Jinsi ya kutumia Kalenda ya Kiuchumi

Unaweza kuweka mapendeleo kwa mwonekano wako kwa kuchagua instruments nyingi za biashara kutoka kwenye orodha kunjuzi ya Ishara.

Ikumbukwe kwamba idadi ya zana za kutrade katika kalenda hubadilika sana, na hutegemea idadi ya matukio na habari zijazo.


Jinsi ya kusoma Kalenda ya Kiuchumi

Baada ya kuchagua instruments unazotaka, utaona orodha ya matukio yanayoonyeshwa kwenye kalenda.

Kuna takwimu mbili muhimu kwenye jedwali, ambazo ni nambari za ‘Actual’ na ‘Forecast’. Tofauti kubwa kati ya nambari hizi mbili inaonyesha kuwa kunaweza kuwa na kubadilikabadilika ghafla katika chati ya zana zinazohusiana za kutrade. Kwa ujumla, kubadilikabadilika ghafla huongezeka dakika 15 kabla ya tukio na hutulia dakika 15 baada ya tukio.

Maswali yanayoulizwa sana

Kalenda ya Kiuchumi huangazia matukio muhimu kutoka kwa uchumi na siasa za kitaifa na kimataifa, ambazo zinaweza kuwa na athari kubwa kwa mabadiliko za bei ya instruments za kutrade.

Huku ikisasishwa kiotomatiki, kalenda huruhusu traders kufahamu na kusasisha matukio yajayo ambayo yanaweza kuathiri trades zao.

Matukio katika Kalenda ya Kiuchumi ndiyo vichochezi vikuu vya kubadilikabadilika ghafla kwa soko, na mara nyingi huratibiwa kutolewa na ripoti, kama vile:

  • Index ya Bei ya Watumiaji (CPI)

  • Kiwango cha ukosefu wa ajira

  • Matangazo ya Pato la Taifa

  • Uamuzi wa kiwango cha riba cha Benki Kuu

  • Data ya Malipo Yasiyo ya Kilimo (NFP)

Kalenda hii huorodhesha matukio yajayo ambayo yanaweza kuathiri mienendo ya financial instruments. Kwa hivyo, traders huona ni muhimu kutumia kalenda ili kusasisha habari za hivi punde na matukio katika nchi kote ulimwenguni.

Matukio haya mara nyingi huratibiwa na yanaweza kutabirika, hivyo basi kuruhusu traders kujua uwezekano wa athari zao kwenye instruments. Wanaweza pia kuzitumia kama viashirio ili kuongeza uwezekano na fursa za kufanya trade.

Kalenda ya Kiuchumi huchukuliwa kuwa muhimu kwa traders wanaofanya trade kupitia uchanganuzi wa kimsingi. Hata hivyo, ni muhimu vile vile kwa traders wote kuangalia kwa umakini kubadilikabadilika ghafla kwa soko ili kuepuka mambo wasiyoyatarajia.

Boresha jinsi unafanya biashara

Jionee mwenyewe kwa nini Exness ndiye broker anayefaa zaidi kwa traders zaidi ya 800,000 na washirika 64,000.